Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
CCM ILIJIPANGA, TULIWEKA MAWAKALA NCHI NZIMA - CPA MAKALLA.
Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam akipokea taarifa ya uandishwaji wa Wananchi kwenye daftari la Mkazi amesema Chama cha Mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kupata taarifa kutokana na kujipanga tofauti na wengine kwanza suala la kuweka mawakala kila eneo kwenye Nchi hii imefanya Chama kifahamu ukubwa wake na kutoa somo kwa wengine.
"Msingi uliofanya CCM uendelee kufatilia Vizuri zoezi hili ni kuweka mawakala kila maeneo wenzetu hawakuwa na na mawakala kila maeneo"
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.