Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KUKUBALIKA KWA SERIKALI YA CCM NA UTEKELEZAJI MZURI WA ILANI YA UCHAGUZI VIMECHOCHEA MWITIKIO KWA WANANCHI KUJIANDIKISHA- CPA MAKALLA
Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam akipokea taarifa ya zoezi la uandikishaji wa daftari la Mkazi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Dar es salaam amesema taarifa iliyotangazwa na Waziri wa Tamisemi hakushangaa kwani takwimu ndani ya Chama zinaonyesha kumekuwa na muitikio mkubwa ni kwa sababu ya kukubalika kwa CCM hasa utekelezaji wa Ilani mzuri ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi hilo halina kificho na Watanzania wanaona .
"Miradi hii haitekelezwi hewani, miradi hii ya Zahanati, madarasa, vituo vya afya inatekelezwa katika maeneo ya vitongoji, vijiji na mitaa kwa hiyo wananchi wa Tanzania wanaona hivi vitu, wanaona namna ambavyo Rais Samia (Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa) amevunja rekodi ya kupeleka fedha za maendeleo katika kila eneo, na kwa maana hiyo wamevutiwa sasa kuona wanaweza wakawasimamia viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaopelekewa fedha hizo ili kuona maendeleo yanaendelea kuwepo kwenye vijiji na mitaa yao ndio maana kuwekuwa na muamko huu" -Makalla
#KaziIendelee
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.