Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KILIMANJARO YAITIKA UFUNGUZI KAMPENI YA CCM SERIKALI ZA MITAA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Rabia Abdalla Hamid amezindua rasmi kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 20, 2024 katika Viwanja vya Bomambuzi, Moshi Mjini, Mkoa wa Kilimanjaro.
Ndg. Rabia amewaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM kwa kuwa wamekidhi sifa za uongozi na wamebeba ajenda halisi za maendeleo.
Amesema Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeleta maendeleo makubwa katika vitongoji, vijiji, mitaa na taifa kwa jumla, hivyo ni muhimu kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi huo ili wakashiriki kwenda kusimamia maendeleo.
Aidha, ameomba wanachama wa CCM kuunganisha nguvu katika kipindi hiki cha kampeini na kuhakikisha ushindi mkubwa unapatikana itakapofika Novemba 27, 2024 siku ya kupiga kura.
Ndg. Rabia ameeleza umuhimu wa serikali za mitaa kama sehemu ambayo wananchi huwasilisha changamoto zao kwenda serikalini kwa ajili ya kupata ufumbuzi.
Amewasihi wananchi kujitokeza kupiga kura na kukichagua Chama Cha Mapinduzi ili kuendeleza kazi kubwa ambazo zimefanyika na zinazoendelea kufanyika za kuwaletea wananchi maendeleo.
#Chamakipokazini.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.