Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MAKAMO WA PILI AKIZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema kampeni ya huduma ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia inalenga kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria Nchini.
Ameyasema hayo wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Mjini Magharibi katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar tarehe 6 june.
Ameeleza kuwa kampeni hiyo itaimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wasiojiweza ,wanawake, watoto pamoja na makundi mengine yanayoishi katika mazingira magumu ,kuimarisha amani na utulivu na kuleta utengamano wa Kitaifa.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewaagiza wanaohusika na utekelezaji wa Kampeni hiyo kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi za kupiga vita na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, udhalilishaji na migogoro ya ardhi vitendo ambavyo vimekua vikijitokeza katika jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaagiza viongozi wa Serikali ya Mkoa wakiwemo Madiwani na Masheha kuwa mabalozi wazuri katika kupiga vita vitendo vya kikatili kwa kusimamia haki na sheria katika kufanya maamuzi.
Aidha Mhe. Hemed amewapongeza wasaidizi wa kisheria Nchini kwa kuendelea kuwasaidia wananchi wasiojiweza ili kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.
Aidha amewapongeza wadau mbali mbali wakiwemo Jeshi la Polisi, Mahkama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake kwa mujibu wa Sheria juhudi ambazo zinaleta taswira njema kwa Wananchi kuwa na imani na wadau hao.
Nae waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Harun Ali Suleiman amesema Kampeni hiyo itasaidia kupunguza dhulma, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika jamii.
Amesema wananchi wengi wanahitaji msaada wa kisheria ambapo ni wazi kuwa wengi wamenufaika na msaada huo wakiwemo wazee wanaofatilia kiinua Mgongo na Pensheni jamii.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idriss Kitwana Mustafa amesema Serikali ya Mkoa itakuwa karibu na wananchi katika kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa ipasavyo kwa lengo la kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia imezinduliwa leo kwa lengo la kuwafikia wananchi hasa wasio na uwezo ikiwa na kauli mbiu isemeyo "Msaada wa kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo "
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.