Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS SAMIA AMEAMUA KUIFUNGUA MIKOA YA KUSINI KIUCHUMI

alternative

Ni barabara ya uchumi Mtwara- Tandahimba- Newala- masasi( 210Km)

MTWARA: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla Rais Samia  Suluhu Hassan ameamua kuifungua mikoa ya Kusini kiuchumi kwa kutenga kiasi cha Sh bilioni 234 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kiuchumi yenye umbali wa kilometa 210.

Makalla alieleza hayo leo Aprili 15,2025 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 10 mkoa wa Lindi na Mtwara.

Aidha, Makalla amesema kuwa Rais Samia amemtuma apite kukagua barabara hiyo ambayo imetajwa kuwa ya kiuchumi na kueleza kuwa hadi sasa kilometa 50 tayari zimekamilika na alijiridhisha kuwa ujenzi bado unaendelea kufanyika kwani amewakuta wakandarasi wakiendelea na maandalizi ya kuikamilisha.

Makalla amesema kuwa Rais Samia anania njema na wananchi wa Kusini mwa Tanzania na katika kutaka kuiimarisha mikoa hiyo kiuchumi ametenga kiasi hicho cha fedha  kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo itakayosaidia katika kuendeleza uchumi.

Akifafanua sababu za barabara hiyo kuwa ya kiuchumi Makalla alisema Rais Samia amefungua mikoa hiyo akiwa na lengo la kuiboresha iweze kukua kwa kuanza na kutoa kiasi cha Sh bilioni 157 kwa ajili kuboresha na kupanua bandari ya Mtwara ambayo itasaidia na kurahisisha usafirishaji wa Korosho kutoka Mtwara kwenda katika maeneo mengine.

Pia amesema kuwa hapo awali Rais Samia alifika Mtwara na kuweka jiwe la msingi katika barabara hiyo inayotoka Newala, Tandahimba hadi Masasi ambayo inakwenda kuunganisha Mtwara na maeneo mengine ya Mchuchuma na Mbamba Bay ambayo.

“Rais Samia amenituma, Mwenezi ukienda huko ukague na hiyo barabara ya kilometa 210, kilometa 50 zipo tayari angalia kama ujenzi unaendelea nimethibitisha nimempita mkandarasi maandalizi yanafanyika vipande viwili kilometa 100 amepewa mkandarasi mmoja, kilometa 60 kapewa mwingine zote 210 mpaka Masasi zinajengwa,” amesema Makalla.

Ameongeza kuwa ili bandari iweze kufanya kazi vizuri na kuleta tija ni baada ya kukamilika kwa barabara hiyo ambayo kusaidia kuimarika kwa uchumi katika mikoa yote ya kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma itakuwa imefunguka vizuri.

alternative
Habari Nyingine