Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
SIMIYU NA CCM, NCHIMBI AKIWASILI ITILIMA
Mapokezi makubwa wananchi na wanaCCM wa Itilima wakimpatia mapokezi makubwa Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi alipowasili eneo la Lugulu kwa ajili ya kuwasalimia, akiwa njiani kuelekea wilayani Maswa, leo tarehe 8 Oktoba 2024, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoa wa Simiyu, ambayo ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Makalla na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.