Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


TANZANIA NI SALAMA CHINI YA RAIS SAMIA

alternative

 

•Nchi yetu ni salama, mipaka yetu ni salama chini ya  uongozi wa Dr Samia

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema kuwa hali ya usalama Tanzania ipo shwari chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Makalla ameeleza hayo leo akiwasalimu wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Tandahimba, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 10 mkoa wa Lindi na Mtwara.

Makalla ameeleza kuwa katika mipaka ya Tanzania ni salama na amepita Nanyamba kuelekea Tandahimba ameona hali ya nchi ni salama na ili maendeleo yapatikane lazima kuwe na amani na utulivu na katika hilo Rais Samia ameifanya kazi hiyo vizuri sana.

“Dk Samia Suluhu Hassan ndiye amiri jeshi wetu Mkuu na yeye bado ametuhakikishia Tanzania ni salama na mimi nashuhudia napita katika mipaka yetu hii tunatoka Nanyamba tunaenda Tandahimba, Newala mpaka Masasi Tanzania ni salama wananchi wetu wanapenda amani na utulivu,” amesema Makalla.

Ameongeza kwa kuwataka wananchi waendelee kushirikiana na serikali na wayalinde mapinduzi na maendeleo yaliyofanyika kwa wivu mkubwa hususani mapinduzi yaliyofanyika katika zao la korosho yalindwe.

alternative
Habari Nyingine