Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewapongeza Wananchi wa Jimbo la Kwahani kwa kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Mgombea wa Chama hicho kuwa Mbunge Mteule Khamis Yussuf Mussa (Pele) kwa ushindi wa kura 7,092
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis mara baada ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kwahani.
Amesema CCM Zanzibar itaendelea kuthamini na kuenzi maamuzi ya Wananchi wa Jimbo hilo walioamua kutumia haki yao ya kidemokrasia kuichagua CCM iendeleze Mapinduzi ya kisiasa katika utekelezaji wa Ilani yake ya mwaka 2020/2025 kwa vitendo.
Katika maelezo yake Mbeto, amewapongeza pia Wogombea wa Vyama vyote vya Siasa nchini vilivyoshiriki Uchaguzi huo na kwamba CCM itaendelea kushirikiana na Vyama hivyo katika kuimarisha demokrasia nchini.
"Tunawashukru sana Wananchi wa Jimbo la Kwahani kwa maamuzi yetu ya kudhibitishia Dunia kuwa Jimbo lenu ni ngome ya CCM kabla na baada ya mfumo wa Vyama vingi vya Siasa Tanzania.
Mbunge mteule mliyemchagua ataendelea kuwasaidia kwa ufanisi Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi katika kujenga na kuimarisha maendeleo ya Jimbo."amefafanua Mbeto.
Sambamba na hayo amempongeza Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Khamis Yussuf Mussa(Pele) kwa ushindi wa kishindo alioupata kupitia Uchaguzi huru na haki uliofanyika katika hali ya Amani na Utulivu.
Pamoja na hayo Katibu huyo Mbeto, alimsisitiza Mbunge huyo mteule Khamis (Pele) kuwa atekeleze kwa vitendo ahadi zote alizoahidi kwa Wananchi wa Jimbo hilo ili waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Katika Uchaguzi huo mdogo jumla ya Vyama vya Siasa 14 vimeshiriki Uchaguzi huo wa Jimbo la Kwahani ambavyo ni CCM kura 7,092, ADA-TADEA kura 49,ADC kura 83, AAFP kura 6,CCK kura 21, CUF kura 79,Demokrasia Makini kura 14, DP kura 7,NRA kura 5, NLD kura 8, SAU kura 7, UNP kura 1,UMD kura 5 na UPDP kura 6.
Uchaguzi huo mdogo uliofanyika leo Juni 8,mwaka 2014 umetokana kufariki Dunia kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ahmada Yahya Abdul-wakil (Shaa) mnamo April 8,2024.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.