Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango mkubwa Unaotolewa na Mashirika ya Umma na itaendelea kuchukua juhudi mbali mbali ili kuhakikisha Mashirika hayo yanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa hapa nchini.
Ameyasema hayo katika hafla ya ufungaji wa wiki ya Mashirika ya Umma Zanzibar iliyofayika katika Kiwanja cha Mapinduzi Square Michenzani jijini Zanzibar.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa Mashirika ya Umma Serikali imechukua hatua ya kuanzishwa kwa Afisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar chini ya Sheria Namba 6 ya mwaka 2021 na kupewa jukumu la kuwa msimamizi mkuu na mmiliki pekee wa uwekezaji wa Mashirika ya Umma kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwepo kwa Afisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar kumechangia kuleta mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa Mashirika ya Umma, utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia kuongezeka kwa kwa mapato ya Serikali ambapo kwa mwaka 2022- 2023 Mashirika ya Umma yameweza kuchangia gawio la Shilingi za Kitanzania Bilioni 13.7.
Mhe.Hemed amesema Shirika la Bandari limeweza kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa meli za mizigo katika bandari ya Malindi kupitia muwekezaji Afrikan Global Logistic(AGL) na kuchochea kuongezeka kwa mapato kutoka shilingi za Kitanzania Bilioni 5.5 hadi kufikia Bilioni 6 kwa mwezi kwa mwaka 2024.
Aidha, Mhe Hemed amefahamisha kuwa Shirika la Bima la Zanzibar limepata mafanikio makubwa kwa kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi kwa kupitia Mifumo ya Tehama na kuchangia kukua kwa mapato kutoka Bilioni 19 kwa mwaka 2021 na kufikia Bilioni 130.74 kwa mwaka 2024.
Sambamba na hayo amewaagiza viongozi wa Mashirika ya Umma kuendelea kuboresha Mifumo ya utendaji katika utoaji wa huduma ili kuleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu na kuendelea kukuza ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na Afisi ya msajili wa Hazina kwa kutatua chamgamoto mbali mbali zinapotokezea.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Dkt. Saada Salum Mkuya amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwenye Mashirika ya Umma hasa katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuhakikisha yanakamilisha malengo na mikakati ya Serikali iliyojiwekea.
Dkt. Mkuya amesema azma ya Rais Dkt. Mwinyi ni kuhakikisha kupitia Shirika la Nyumba na Mashirika mengine Zanzibar inakuwa na mji wenye majengo ya kisasa yenye kukidhi huduma zote stahiki ambayo yataufanya Mji wa Zanzibar kuwa wenye haiba na muonekano mzuri utakaoitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi.
Dkt. Saada amewataka wananchi kupuuza uvumi unaotolewa na wasioitakia mema Zanzibar na badala yake kuyatangaza mambo mazuri ya kimaendeleo yanayofanywa na Rais Dkt Hussein Mwinyi kwa Wazanzibari wote.
Kwa upande wake Msajili wa Hazina Zanzibar Bwana WAHIDI MOHAMMED SANYA amesema Afisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar imefanikiwa kuyaunganisha Mashirika 18 ya Umma yaliyopo Zanzibar ambayo yanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa jambo ambalo linaifanya Afisi ya Msajili wa Hazina kupiga hatua kimaendeleo katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake.
Bwana. WAHIDI amesema Wiki ya Mashirika ya Umma itakuwa endelevu na itafanyika kila mwaka lengo ikiwa ni kuyaweka pamoja Mashirika na kujadili mafanikio lakini pia kutafuta njia muafaka za kupata utatuzi wa changamoto mbali mbali zinazoyakabili mashirika hayo.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea mabanda ya maonesho ya Mashirika ya Umma yaliyojotokeza katika kuadhimisha Wiki ya Mashirika ya Umma Zanzibar iliyofayika katika Kiwanja cha Mapinduzi Square Michenzani jijini Zanzibar.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.