Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

alternative

Hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya vyama sita rafiki vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika imefanyika leo katika Mwalimu Julius Nyerere Leadership School. Vyama vinavyoshiriki katika mafunzo hayo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ZANU–PF, African National Congress (ANC), SWAPO, FRELIMO pamoja na MPLA, vikilenga kuendelea kuimarisha mshikamano na misingi ya uongozi wa vyama vya ukombozi barani Afrika. Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi leo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Stephen Masato Wasira, ambapo yatafanyika kuanzia tarehe 18 Mei hadi 25 Mei 2026 kwa lengo la kuwajengea washiriki uwezo wa kiuongozi, usimamizi na kuendeleza tunu za harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. #CCM #ZANUPF #ANC #SWAPO #FRELIMO #MPLA #Leadership #AfricanLiberationMovements #MwalimuNyerereLeadershipSchool

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine