Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈

alternative

HAI - KILIMANJARO: Ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi Kwa Sadala umeondoa changamoto ya wanafunzi kutembea zaidi ya kilomita 12 kufuata elimu, huku ukipunguza hatari za ajali na vifo vilivyokuwa vikisababishwa na umbali mrefu wa kufika shuleni. Akikagua mradi huo wenye thamani ya Sh milioni 351.5, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha sekta ya elimu na kuwasogezea wananchi huduma muhimu karibu yao. Mradi huo umejumuisha madarasa ya shule ya msingi na awali, jengo la utawala pamoja na vyoo, na umeboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji huku ukichochea maendeleo ya jamii kwa ujumla. ____________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #MaendeleoYaElimu #CCMIpoKazini #KaziInaendelea

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine