Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐍𝐈 ππ™π€πŒπ” π˜π€ πŒπŠπŽπ€ 𝐖𝐀 πŒπ€ππ˜π€π‘π€!

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Laban Kihongosi, anatarajia kuanza ziara yake rasmi mkoani Manyara tarehe 01 Juni, 2026. Ziara hii inalenga kuimarisha chama, kusikiliza wananchi, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kusikiliza na kupokea changamoto mbalimbali za wananchi ili kuendelea kuharakisha maendeleo ya Mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla. Wananchi wa Manyara wamejipanga kumpokea kwa hamasa kubwa kiongozi huyu ambaye ameendelea kuwa sauti ya chama katika kuhimiza umoja, mshikamano na uwajibikaji. Chini ya CCM, maendeleo yanaendelea kupatikana na matumaini ya wananchi yanaendelea kuimarika kila siku. πŸ“’Manyara mko tayari??? MTUMISHI WA WOTE NDUGU KENANI LABAN KIHONGOSI ______________ #KazinNaUtuTunasongaMbele! #KenaniKihongosiManyara #CCMKaziNaUtu

alternative
Habari Nyingine