Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔

alternative

𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔 KILIMANJARO: RAIS Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amempatia bajaji Mkazi wa Kata ya Sanya Juu, wilayani Siha, Yahaya Lema maarufu ‘2Pac’ ambaye ni mlemavu wa miguu, kwa lengo la kumwezesha kujishughulisha na shughuli za kiuchumi. Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi amemkabidhi Lema bajaji yake leo Mei 30, 2026 baada ya kuwasilisha ombi la mkazi huyo aliloliwasilisha kwake Mei 26, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi Sanya Juu wilayani Siha. Akizungumza wakati wa kumkabidhi Lema bajaji yake, Kihongosi amesema baada ya kupokea ombi la Lema alimfikishia suala hilo kwa Rais Samia ambaye alikubali kumsaidia kupata bajaji kwa ajili ya kujiongezea kipato. “Bajaji hii mpya ameitoa Mheshimiwa Rais kwa ajili ya ndugu yetu. Kwa niaba yake, ninamkabidhi pamoja na nyaraka zote za malipo na umiliki wake,” amesema Kihongosi. Aidha, aliwataka viongozi wa Serikali na CCM wilayani Siha kuhakikisha wanamsimamia na kumsaidia mnufaika huyo ili aitumie fursa hiyo kwa maendeleo yake na ya familia yake. Hatua hiyo imeweka wazi jitihada za Serikali ya CCM pamoja na chama kwa ujumla za kuwainua wananchi wenye mahitaji maalumu kwa kuwapatia fursa za kujitegemea kiuchumi badala ya kutegemea misaada, sambamba na kuimarisha ustawi wa familia zao na jamii kwa ujumla. Wananchi wa eneo hilo wamepongeza kitendo hicho wakieleza kuwa ni kielelezo cha utekelezaji wa dhana ya Kazi na Utu, kwani mbali na kusikiliza changamoto zao, viongozi wanachukua hatua za kuzitatua kwa vitendo na kuleta matumaini mapya kwa makundi mbalimbali ya kijamii. __________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #MaendeleoKwaWote

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine