π°VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dkt. Mohamed Dimwa Leo tarehe 23 Mei 2026 amehitimisha mafunzo maalum yaliyokuwa yakifanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Mei 2026 kwa viongozi kutoka vyama sita rafiki vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambavyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM - Tanzania), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), na African National Congress (ANC - Afrika Kusini). Mafunzo hayo yamehitishwa hapo jana trh 23 Mei, 2026 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Leadership School uliopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Mafunzo hayo yaliyoongozwa na kaulimbiu isemayo, βKusalia Waaminifu kwa Misingi na Dhima Yetu ya Awali, Tukisonga Mbele Pamoja Kuelekea Maendeleo ya Kisasa,β yameelezwa kuwa yamekuja katika wakati muafaka ambapo dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yanayohitaji uimara wa misingi ya vyama vya ukombozi. Viongozi walisisitiza kuwa vyama hivi vina wajibu mkubwa wa kuendelea kulinda mamlaka ya wananchi, kuimarisha mshikamano wa kikanda, na kuhakikisha maendeleo ya nchi zao yanaendelea kujengwa kwa misingi ya uhuru, utu, uzalendo na kujitegemea bila kuendeshwa na misukumo ya kimagharibi inayoweza kupotosha dira ya mataifa yao. Aidha, Dkt. Dimwa ameelezwa kuwa kupitia mafunzo haya na ushirikiano wa kimkakati baina ya vyama hivyo, juhudi zaidi zitaelekezwa katika kuimarisha ideolojia, kukuza uongozi wenye maadili, na kujenga kizazi kipya cha viongozi watakaolinda historia, misingi na malengo ya vyama vya ukombozi vilivyopigania uhuru wa mataifa yao. Viongozi hao wameahidi kuendeleza mshikamano huo wa kihistoria kwa vitendo, wakiamini kuwa umoja wao ndio nguzo ya kudumu ya maendeleo, amani na ustawi wa Kusini mwa Afrika. π : Mei 23, 2026 π: Kibaha, Zanzibar #ccm_zanzibar #ccm_tanzania #vitendovinasauti #yajayoneemazaid
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
24-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE β KIBAHA
24-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
24-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
24-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
24-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
24-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
24-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
24-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
24-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
24-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
24-05-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
24-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
24-05-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
24-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
24-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
24-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
24-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
24-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
24-05-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
24-05-2026