Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO

alternative

MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO Mapokezi ya kihistoria na yenye hamasa kubwa yaliyotokea Leo tarehe 29 Mei 2026 Mkoa wa Kilimanjaro kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Laban Kihongosi, aliyewasili rasmi kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo. Wanachama wa CCM, viongozi wa chama na serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro wamejitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo, jambo lililoonesha mshikamano, uhai wa chama na imani kubwa ya wananchi kwa CCM na uongozi wake. Ziara hiyo inalenga kuimarisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, kukagua shughuli za chama, kuzungumza na wanachama pamoja na kuendelea kuhamasisha uwajibikaji, uzalendo na maendeleo kwa wananchi. CCM inaendelea kusonga mbele kwa nguvu, umoja na mshikamano chini ya viongozi wake madhubuti. #KaziNaUtuTunasongaMbele #ZiaraYaKazi #mtumishiwawote

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine