Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


πŒπ‡π„. π‘π€πˆπ’ 𝐀𝐍𝐀𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐀𝐍𝐀 π–π€π“π€ππ™π€ππˆπ€, π–π€π“π”πŒπˆπ’π‡πˆ 𝐖𝐀 π”πŒπŒπ€ π“πˆπŒπˆπ™π„ππˆ π–π€π‰πˆππ” 𝐖𝐄𝐍𝐔 πŠπˆπŠπ€πŒπˆπ‹πˆπ…π”: π‘π€ππˆπ€

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, amewataka watumishi wa umma kote nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwajibikaji na weledi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati. Akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii mkoani Mtwara, Ndugu Rabia amesema dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuona kila Mtanzania anahudumiwa kwa haki, usawa na bila vikwazo visivyo vya lazima. β€œWananchi wanahitaji huduma bora. Watumishi wa umma wanapaswa kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto za wananchi na si sehemu ya changamoto hizo. Tuwahudumie Watanzania kwa uaminifu, weledi na heshima,” amesema Rabia. Tembelea: www.ccm.or.tz _________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMTabasamuLaWatanzania #CCMIpokazini!

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine