Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!

alternative

Shilingi milioni 500 zimeahidiwa na Waziri wa Maji, Ndugu Jumaa Aweso, kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Hatua hiyo imefuatia mawasiliano ya simu kati ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, na Waziri huyo, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa CCM kusogeza ufumbuzi wa haraka wa changamoto za wananchi. Wananchi wa Kilolo wameendelea kufurahia matokeo ya ufuatiliaji wa karibu wa CCM katika kuboresha huduma za maji na maisha ya jamii. Tembelea: www.ccm.or.tz _________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #SimuImeita #Kilolo

alternative
Habari Nyingine