Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesema kukamilika kwa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa Wilaya ya Kilolo kutafungua fursa kubwa za ajira na kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi. Kihongosi ameyasema hayo leo, Juni 19, 2026, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho katika Kijiji cha Luhindo, Kata ya Mtitu, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Akizungumza baada ya ukaguzi huo, amesema chuo hicho kitawajengea vijana ujuzi wa kujiajiri na kuajirika katika sekta mbalimbali za uzalishaji. "Kukamilika kwa mradi huu kutaleta fursa kubwa kwa vijana wetu kupata mafunzo yatakayowasaidia katika masuala ya ajira, huku Halmashauri ikinufaika na wataalamu watakaozalishwa kupitia mafunzo hayo," amesema Kihongosi. Ameongeza kuwa uwepo wa karakana tatu utasaidia utoaji wa mafunzo ya vitendo yatakayowawezesha vijana kujipatia kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi wa familia zao na Taifa kwa ujumla. Aidha, amesema CCM na Serikali vitaendelea kushirikiana kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili wananchi wa Kilolo wanufaike kikamilifu na uwekezaji huo. Awali, Mdhibiti Ubora wa Shule, Altos Kinunda, amesema chuo hicho kinatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.6. Hadi sasa, kimepokea shilingi milioni 777.4, ambapo shilingi milioni 573.7 zimetumika na shilingi milioni 203.7 zimebaki kwa ajili ya kuendeleza ujenzi. Amesema awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa majengo tisa, ikiwemo jengo la utawala, madarasa, karakana, nyumba ya mtumishi, jengo la mlinzi na jengo la umeme. Ujenzi umefikia asilimia 76 na ukikamilika chuo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 240. Tembelea: www.ccm.or.tz _____________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #VETAKilolo

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine