INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
-Asisitiza mabalozi kupandisha bendera za chama kwenye maeneo yao. -Asema chama kinawajali na kuwathamini mabalozi. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amesema maendeleo ya kweli kwa wananchi huanzia katika mashina ya Chama hicho, akisisitiza kuwa jitihada zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupata nguvu kupitia uongozi wa ngazi za chini. Dkt. Migiro ambaye ni Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke tangu chama hicho kianzishwe, amesema hayo katika mkutano wake na Mabalozi wa Mashina wa CCM katika Wilaya ya Ilala, ikiwa ni hitimisho la ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam yenye lengo la kuimarisha uhai wa CCM kuanzia kwenye mashina Kwa kauli mbiu ya "Shina lako linakuita". Akizungumza na Mabalozi hao amesema mashina ndiyo sehemu ya kwanza ya wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo, kwa kuwa ndiko wanakotoka wananchi wenyewe na ndiko changamoto zao halisi zinapojadiliwa. Ameeleza kuwa mahusiano kati ya maendeleo ya jamii na maendeleo ya kisiasa hayawezi kutenganishwa, kwa kuwa mashina imara huwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji, jambo linaloongeza imani ya wananchi kwa Chama. Ameongeza kuwa viongozi wa mashina wana wajibu mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, akisema uangalizi wa karibu wa miradi hiyo ndio msingi wa maendeleo yenye tija kwa wananchi. Aidha, Mwanadiplomasia huyo, amesema Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongeza kazi kubwa inayofanywa na mabalozi hao wa mashina na kwamba chama kitaendelea kuthamini mchango wao mkubwa kwenye mashina.
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
29-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
29-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
29-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
29-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
29-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
29-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
29-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
29-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
29-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
29-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
29-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
29-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
29-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
29-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
29-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
29-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
29-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
29-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
29-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
29-05-2026