Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐓𝐇𝐈𝐁𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐓𝐀𝐖𝐀𝐋𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ameshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Botswana National Front (BNF) unaofanyika mjini Jwaneng, Botswana, akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Rabia amesisitiza kuwa vyama tawala vina wajibu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, kuimarisha misingi ya utawala bora na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi mahitaji ya wananchi. Aidha, amekihimiza Chama cha BNF kuendelea kuweka maslahi ya wananchi mbele katika utekelezaji wa sera na maamuzi yake, ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayebaki nyuma katika mchakato wa maendeleo ya Taifa. Ndugu Rabia amempongeza Rais wa BNF na Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mhe. Duma Gideon Boko, kwa ushindi wa Chama hicho na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Botswana, akieleza kuwa ushindi huo ni kielelezo cha imani waliyopewa na wananchi. Amewatakia Rais Boko na Chama cha BNF mafanikio katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo na ustawi. Tembelea: www.ccm.or.tz __________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini

alternative alternative
Habari Nyingine