Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐕𝐈𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐕𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐌𝐈𝐈 𝐋𝐈𝐍𝐃𝐈 𝐕Y𝐀𝐌𝐒𝐇𝐔𝐊𝐔𝐑𝐔 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐈𝐒𝐈𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐑𝐈𝐁𝐀

alternative

Tarehe 14 Juni, 2026, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, alipokea salamu za pongezi na shukrani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya kijamii mkoani Lindi vilivyonufaika na mikopo ya serikali isiyo na riba. Vikundi hivyo vimesema mikopo hiyo imewasaidia kuimarisha shughuli zao za kiuchumi na kuboresha kipato cha kaya zao, huku wakitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ndugu Rabia alitembelea pia maeneo ya kazi ya vikundi hivyo ili kujionea maendeleo yao na kusikiliza uzoefu wao katika utekelezaji wa shughuli za kujipatia kipato. Tembelea: www.ccm.or.tz __________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMTabasamuLaKilaMtanzania #CcmIpoKazini

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine