Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, ametembelea Kituo cha Afya Kaloleni jijini Arusha na kujionea huduma zinazotolewa pamoja na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Watumishi wa afya katika kituo hicho wamemshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya kupitia uboreshaji wa miundombinu, upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa na mazingira bora ya utoaji huduma kwa wananchi. Akizungumza na watumishi hao, Ndugu Kihongosi amewapongeza kwa uzalendo, weledi na kujituma kwao katika kuwahudumia wananchi, akisisitiza kuwa huduma bora wanazozitoa ni ushahidi wa mafanikio ya Serikali na sababu kubwa inayozidi kujenga imani ya wananchi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema matokeo ya kazi nzuri katika vituo vya afya, hospitali, shule na maeneo mengine ya utoaji huduma za kijamii ndiyo kioo kinachoonesha utekelezaji wa Ilani ya CCM na dhamira ya Serikali ya kuboresha maisha ya Watanzania. Katika kuonesha mshikamano na kuguswa na changamoto ya mgonjwa aliyekuwa akihitaji msaada wa matibabu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msaada wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ya kuchangia gharama za matibabu yake. "Huduma bora kwa wananchi ndiyo sura halisi ya maendeleo na msingi wa imani ya wananchi kwa Serikali yao." MTUMISHI WA WOTE Tembelea: www.ccm.or.tz __________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #MtumishiWaWote

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine