Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐅𝐈𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎, 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐘𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐎𝐇𝐀𝐌𝐀𝐒𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐍𝐉𝐈𝐅𝐔 𝐖𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesema CCM imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Ndugu Kihongosi amesema maendeleo yanayoonekana katika sekta za afya, elimu, maji, umeme, miundombinu na uwezeshaji wa wananchi ni matokeo ya utekelezaji thabiti wa sera na mipango ya Serikali. Amesisitiza kuwa amani, umoja na mshikamano ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa, huku akionya dhidi ya vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi na kuathiri safari ya maendeleo ya wananchi. Tembelea: www.ccm.or.tz __________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #MtumishiWaWote

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine