Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amewataka wananchi wa Arusha kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa kwa kutokubali kushawishiwa na siasa za chuki, migawanyiko na maandamano yasiyo na tija kwa maendeleo ya wananchi. Akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Shina la Wakereketwa Noah Saccos, Arusha Mjini, Ndugu Kihongosi amesema nguvu za vijana na wananchi zinapaswa kuelekezwa katika uzalishaji, ujasiriamali na kushiriki kikamilifu katika fursa zinazotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesisitiza kuwa Arusha ina kila sababu ya kujivunia mafanikio ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika sekta mbalimbali, huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kushiriki katika kujenga uchumi imara kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. "Maendeleo yanajengwa kwa kazi, umoja na amani; si kwa migogoro na maandamano." MTUMISHI WA WOTE Tembelea: www.ccm.co.tz ________________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #MtumishiWaWote #CCMIpoKazini #ArushaMjini

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine