Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR

alternative

Leo, tarehe 8 Septemba 2025, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Migiro amemfikishia Dkt. Mwinyi salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mgombea wa Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Dkt. Migiro amempongeza Dkt. Mwinyi kwa kuaminiwa tena na kuteuliwa na Chama kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar.

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine