Kuhusu CCM

Historia, imani, malengo, itikadi na muundo wa Chama Cha Mapinduzi—chama kiongozi cha ukombozi kinachounganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Kuanzishwa

1977

5 Februari

Muungano

TANU + ASP

Tanzania Bara na Zanzibar

Wanachama

12M+

Chama kikubwa barani Afrika

Urais

Ushindi 6+

Tangu vyama vingi, 1992

Historia ya Chama Cha Mapinduzi

Kuanzishwa kwa CCM, muungano wa TANU na ASP, na safari ya chama tangu 1977.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikubwa zaidi, kikongwe, chenye nguvu na mvuto barani Afrika, kinachoongoza kwa kuwa na wanachama zaidi ya milioni 12. Ni chama kiongozi cha ukombozi kilichoshiriki kupigania uhuru nchi nyingi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara.

CCM kilianzishwa rasmi Februari 5, 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chama tawala Tanzania Bara, kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala Zanzibar, kikiongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume.

CCM imeendelea kushinda chaguzi zote sita za urais tangu kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 1992, huku ikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Viongozi walioshinda urais kwa tiketi ya CCM kwenye chaguzi hizo ni Benjamin Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete, Dkt. John Pombe Magufuli na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

1954

TANU

Tanganyika African National Union inaanzishwa, ikiwa msingi wa ukombozi Tanzania Bara.

1957

ASP

Afro-Shirazi Party inaanzishwa Zanzibar na kuwa chama tawala baada ya mapinduzi.

1977

CCM

TANU na ASP vinaungana rasmi 5 Februari kuunda Chama Cha Mapinduzi.

1992

Vyama vingi

CCM inaendelea kushinda chaguzi za urais tangu mfumo wa vyama vingi.

Wenyeviti wa CCM

Mwenendo wa uongozi wa taifa wa chama tangu kuanzishwa mwaka 1977.

JK

Julius Kambarage Nyerere

1977 — 1990

01
AH

Ali Hassan Mwinyi

1990 — 1996

02
BW

Benjamin William Mkapa

1996 — 2006

03
JM

Jakaya Mrisho Kikwete

2006 — 2016

04
JP

John Pombe Magufuli

2016 — 2021

05
SS

Samia Suluhu Hassan

2021 — sasa

06
Wenyeviti wa CCM tangu 1977

Jumuiya za Chama

CCM inahudumia makundi yote kupitia jumuiya tatu zenye muundo unaofanana na wa chama.