CCM

Chama Cha Mapinduzi

Malengo

Malengo na Madhumuni ya CCM

(1) Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu
na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na
Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa upande
mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili.

(2) Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu
na raia wake.

(3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea
kwa mujibu wa Azimio la Arusha.

(4) Kusimamia utekelezaji wa Siasa ya CCM
pamoja na kuendeleza fikra za viongozi
waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama
zilivyofafanuliwa katika maandiko mbali
mbali ya Vyama hivyo.

(5) Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya
kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha
yake na mali yake kwa mujibu wa sheria

(6) Kuona kwamba katika Nchi yetu kila mtu
aliye na uwezo wa kufanya kazi anafanya
kazi; na kazi maana yake ni shughuli yoyote
halali inayompatia mtu riziki yake

(7) Kusimamia haki na maendeleo ya
Wakulima, Wafanyakazi na wananchi
wengine wenye shughuli halali za
kujitegemea; na hasa kuona kwamba kila
mtu ana haki ya kupata malipo
yanayostahili kutokana na kazi yake

(8) Kuona kwamba kwa kutumia Vikao
vilivyowekwa, raia anayo haki ya kushiriki
kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi wa
mambo ya Taifa na yanayomhusu, na
kwamba anao uhuru wa kutoa mawazo
yake, wa kwenda anakotaka, wa kuamini Dini anayotaka na kukutana na watu
wengine,maadamu havunji Sheria au
Taratibu zilizowekwa

(9) Kuona kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa
misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa

(10) Kuhifadhi, kukuza na kudumisha imani na
moyo wa kimapinduzi miongoni mwa
Watanzania pamoja na ushirikiano na
wanamapinduzi wenzetu kokote waliko

(11) Kuweka na kudumisha heshima ya
binadamu kwa kufuata barabara Kanuni za
Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu.

(12) Kuona kwamba Dola inakuwa Mhimili wa
Uchumi wa Taifa.

(13) Kuona kwamba Serikali na Vyombo vyote vya
Umma vinasaidia kwa vitendo kuanzishwa na
kuendeleza shughuli za Ushirika na za
ujamaa, na shughuli nyinginezo halali za
wananchi za kujitegemea.


(14) Kuona kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa
yanatilia mkazo maendeleo ya Wananchi
na hasa jitihada za kuondosha umasikini,
Ujinga na Maradhi.

(15) Kuona kwamba Serikali na vyombo vyote
vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa
raia wote, wanawake na wanaume bila
kujali rangi, kabila, Dini, au hali ya mtu.


(16) Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna
aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi,
rushwa, uonevu na/au upendeleo.


(17) Kuendelea kupiga vita Ukoloni Mamboleo ubeberu na ubaguzi wa aina yoyote

(18) Kuimarisha uhusiano mwema na Vyama
vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye
itikadi kama ya CCM ambavyo kweli
vinapinga Ukoloni, Ukoloni Mamboleo,
Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.


(19) Kushirikiana na Vyama vingine katika Afrika,
kwa madhumuni ya kuleta umoja wa Afrika,
na kuona kwamba Serikali inaendeleza na
kuimarisha ujirani mwema.

betbaba betbaba giriş betbaba kayıt betist Kadinca forum instagram takipçi hilesi instagram beğeni hilesi instagram free followers instagram takipçi twitter begeni instagram begeni hilesi instagram free followers instagram takipci hilesi instagram giris yap instagram giris yap free follower for instagram free follower for instagram instagram beğeni hilesi instagram beğeni