UKumbi  wa Mikutano wa Chama
UKumbi  wa Mikutano wa Chama
previous arrow
next arrow
Slider

CCM

Chama Cha Mapinduzi

Wabunge watakaozembea kutekeleza ilani ya CCM ‘wataliwa vichwa’ – Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) watakaozembea katika kutekeleza ilani ya CCM, hawatapitishwa na chama hicho kugombea tena katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Polepole ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora.

Polepole amesema ni lazima wabunge watekeleze kwa vitendo ilani ya chama hicho na katika kuweka msisitizo amesema Wabunge watakaozembea kutekeleza ilani ya CCM, ‘wataliwa vichwa’ na yeye akiwa miongoni mwa ‘wala vichwa’.

Hata hivyo, alimpongeza Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM akisema kuwa ni Mbunge anayefanya kazi zake vizuri na kutekeleza vema ilani ya CCM.

Akizungumzia wanachama wanaoanza kujipitisha kutaka kugombea, Polepole amesema wanapaswa kuwaacha waliopo wafanye kazi huku akiwaonya kuwa wanaokiuka taratibu za chama watashughulikiwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama.

Lengo la Mkutano huo ni kusikiliza na kupokea taarifa ya Mbunge kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM.