UKumbi  wa Mikutano wa Chama
UKumbi  wa Mikutano wa Chama
previous arrow
next arrow
Slider

CCM

Chama Cha Mapinduzi

DKT. BASHIRU ATAKA TIJA FURSA ZA MASOMO NJE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally leo amefanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke ambapo ametaka fursa zinazotolewa kwa watanzania kusoma vyuo vya nje zijikite katika teknolojia ya uzalishaji.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu Dodoma pamoja na mambo mengine, yamelenga katika kupanua wigo wa ushirikiano ambapo Dkt. Bashiru ameleeza msimamo wa CCM kuhimiza zaidi kupatikana kwa fursa zenye tija kwa maendeleo ya viwanda hasa zinazolenga mafunzo ya vitendo katika kilimo, ufugaji na viwanda.