ZIARA YA CHONGOLO YAACHA NEEMA KILOSA.
ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo mkoani Morogoro, imeachaneema kwa wakazi wa Wilaya Kilosa baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutangaza gharama yauunganishaji umeme wilayani humo sasa ni sh. 27,000 tu.
Hatua hiyo imetangazwa leo Januari 30, 2023 baada yaKatibu Mkuu Chongolo Meneja wa TANESCO Mkoa waMorogoro Fadhili Chilombe kutoa ufafanuzi dhidi yamalalamiko ya wananchi waliolalamikia kuunganishiwaumeme kwa sh. 310,000.
Akijibu changamoto hiyo baada ya Katibu MkuuChongolo kumtaka afanye hivyo, Chilombealiwahakikishia wananchi kuwa kuanzia leo umemekatika vijiji vya Kilosa ikiwemo Kata ya Dumilautaunganishwa kwa gharama ya sh. 27,000 tu na sio sh. 310,000.
Pia, amemuhakikishia Katibu Mkuu Chongolo kuwa nawananchi kuwa, hadi Aprili mwaka huu, vijiji vyote vyaKilosa vitakuwa vimefikishiwa umeme.
Ufafanuzi huo ulitokana na taarifa ya Katibu wa ShinaNamba 10 Dumila, Zainabu Ajili Ally ambaye ameesemakata hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazozimekuwa adha kwa wananchi, ikiwamo gharama kubwaza uunganishaji wa umeme majumbani.
Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoroakiwa ameongozana na na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu).