Chongolo Akutana na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Reverien Ndikuriyo ....
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo leo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Reverien Ndikuriyo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Viongozi hao wawili kwa pamoja wameridhishwa na mahusiano na ushirikiano mzuri ya Tazania na Burundi.
Na wameahidi kuendelea kushirikiana katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Kiuchumi na Kisiasa.