CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


DKT. BASHIRU AWAHIMIZA WANACCM UDSM KUENZI MIAKA 100 YA FIKRA ZA  MWALIMU

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewahimiza wanaCCM wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kuenzi miaka 100 ya fikra za Mwalimu Nyerere, Aprili 2022.

Ameysema hayo leo tarehe 21 Februari, 2021 akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.

"Mwaka kesho Aprili, Baba wa Taifa Mwl. Nyerere atatimiza miaka 100 ya uhai wake tangu Aprili, 2022 azaliwe mpaka sasa. Kutakua na sherehe kubwa katika nchi yetu, na kwa Chama Chetu lazima tudhihirishe kabisa kwamba tunamuenzi baba wa Taifa mwaka kesho mwezi Aprili."

"Na mimi nipendekeze hapa mbele yenu kwamba, WanaCCM hapa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, muwe mstari wa mbele katika maandalizi ya sherehe hizo, kwa sababu miaka 100 ya utoto wake, malezi yake, maisha yake ya kisiasa, maisha yake ya kiraia, mpaka anafariki na hadi sasa yamebeba urithi mkubwa wa Taifa letu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kikiwepo"

Aidha, Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa Utunzaji wa mazingira kutokana na kutoridhishwa na usafi katika Jiji la Dar es Salaam.

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50