UZINDUZI WA DAYOSISI MPYA YA KATI NA KUMWEKA WAKFU ASKOFU MPYA WA AICT DAYOSISI YA KATI .
Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Dkt. Maudline C. Castico Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo Amehudhuria Ibada ya kumweka Wakfu na Kusimikwa kwa Askofu Amos Katoto Ngeze wa Kanisa la Africa Inland Church ( AICT) Kizota Jijini Dodoma.
Katika Ibada hiyo ya kumweka wakfu na Kumsimika Askofu Amos Ngeze imeambatana na uzinduzi wa Dayosisi Mpya ya Kati Jijini Dodoma.
Hata hivyo Ibada hiyo ya uzinduzi wa Dayosisi Mpya ya Kati imehudhuriwa na Maaskofu kutoka Dayosisi zote za Makanisa ya Africa Inland Church (AICT) wakiongozwa na Askofu Mkuu wa AICT Askofu Mussa Magwesela ambapo Mgeni Rasmi wa Ibada hiyo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt. Angelina S. Mabula iliyofanyika Kizota Mkoani Dodoma.