CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


Ufaransa Yasisitiza Kuendeleza Ushirikiano Na Tanzania Baada Ya Uchaguzi Mkuu..

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bw. Frederic Clavier ambapo Balozi huyo ameeleza kufurahishwa na maendeleo makubwa yanayoendelea kufanyika pamoja na kusisitiza kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 11 Desemba, 2020 Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

"Nchi kwa sasa ina muelekeo mzuri baada ya kufikia hatua ya uchumi wa kati, hivyo ni habari njema kwa watanzania na ni muelekeo mzuri katika mashirikiano ya uwekezaji, na tumevutiwa sana na Hotuba aliyoitoa Mhe. Rais Magufuli jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa bunge la 11 kuhusu mikakati ya ukuzaji wa sekta binafsi nchini." Balozi Frederic Clavier

Balozi ameongeza kuwa, "Baada ya Uchaguzi Mkuu miaka hii mitano ijayo ni miaka ya kufanya kazi, ushindi wa CCM umekuwa mkubwa sana licha ya changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza lakini Uchaguzi umekwisha salama na serikali imeshaundwa na sasa ni muda wa kuchapa kazi na mikakati ya maendeleo ni mizuri na nina imani ushirikiano wetu utaimarika zaidi."

Aidha, Katibu Mkuu ameeleza kuwa, mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa vyuo vya ufundi ili kukuza upatikanaji wa ajira, na pia kuimarisha zaidi sauti ya Tanzania Katika Jumuiya za Kimataifa, kwa kuzingatia kuwa sauti ya Tanzania kihistoria imekuwa kubwa na hasa katika maeneo ya Usalama, Amani na katika Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuchangia Amani Afrika na nje ya Afrika, na CCM itaendelea kuilekeza seriakali kuongeza juhudi katika ushirikiano huo.

Huu ni utaratibu wa Viongozi wa Chama kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine yenye nia njema ya Nchi yetu.

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50