CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CCM TAIFA

alternative

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Kilichoketi leo tarehe 28/02/2020  katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, pamoja na mambo mengine kimepokea taarifa ya Kamati ndogo ya Usalama na Udhibiti juu utekelezaji wa maamuzi ya kuwaita na kuwahoji wanachama wake watatu, ambao ni Yusuph Makamba na Ndg Abdulrahman Kinana (Makatibu wakuu wa CCM wastaafu) pamoja na Ndg Benard Membe, juu ya shutuma za kimaadili zinazowakabili.

Baada ya kupitia taarifa na kujadiliana kwa kina Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwa kauli moja imeazimia yafuatayo:-

1. Kumsamehe Ndg Yusuph Makamba kwa  Makosa yake aliyoyatenda

2. Kumpa karipio Ndg Abdulrahman Kinana kufuatia makosa yake aliyotatenda

3. Kumfukuza uanachama Ndg Benard Membe kufuatia makosa yake aliyoyatenda.

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50