Kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichokutana Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma leo Jumatatu tarehe 26 Septemba, 2022.