MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CCM NDG. DANIEL CHONGOLO WILAYA YA MVOMERO MKOA WA MOROGORO
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Daniel Chongolo akiendelea na ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM na Kusikiliza Kero Mbalimbali za wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro, leo Januari 29, 2023, amepokelewa wilayani Mvomero, akitokea Wilaya ya Gairo. Baada ya mapokezi katika eneo la Dumila, Ndg. Chongolo ameshiriki Mkutano wa Shina. Na. 18, Tawi la Dumila na kukagua ujenzi wa mradi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Dumila.
Katika Ziara hiyo Katibu mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo ameambatana na Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Ndg. Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.