CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


KATIBU WA NEC IDARA YA ORGANAIZESHENI (MCC) NDG. ISSA HAJI USSI (GAVU) AMERIPOTI KATIKA OFISI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI MAKAO MAKUU DODOMA.

alternative

Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Haji Ussi (GAVU) ameripoti leo katika ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma, na kufanya kikao Cha Wakuu wa sehemu na maafisa wa Idara hiyo wakiongozwa na Msaidizi Mkuu wa Idara hiyo Ndg. Solomon Itunda.

Ndg. Issa Haji Gavu amefanya kikao na Maafisa wa Idara hiyo wakijadili masuala mbalimbali ya maandalizi ya vikao Vya Chama pamoja na kutoa shukrani za dhati kwa kikao kilichomteua Cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanya uteuzi wa nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi yake ya Katibu wa NEC Idara ya Organaizeshen kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan.

Ndg. Gavu amekiri kupokea uteuzi huo kwa mikono miwili na kuahidi kufanya kazi kwa Bidii na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakuu wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wote wa Chama na serikali.

Aidha ameomba Ushirikiano katika Kazi kwa Wakuu wa vitengo na Maafisa wa Idara ya Organaizesheni akisisitiza Umoja na majadiliano ndiyo msingi wa mafanikio katika Idara.

alternative alternative alternative

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50