KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA MIWILI (2) YA UONGOZI WA AWAMU YA SITA, MACHI 19, 2023.
Baadhi ya Matukio kutoka uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam leo Machi 19, 2023 ambapo kilele cha Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Uongozi wa Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan yanafanyika na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama ngazi zote, asasi za kiraia na makundi mbalimbali ya wanawake nchini kote.
Rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM Taifa ndiye Mgeni Rasmi wa Kilele cha Maadhimisho haya yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT).