Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Ndg.Christina Mndeme ameendelea na Ziara yake ya siku nne Mkoani Kigoma
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Ndg.Christina Mndeme ameendelea na Ziara yake ya siku nne Mkoani Kigoma ambapo Leo ametembelea Wilaya ya Uvinza na kukagua ujenzi wa tenki la maji katika Kata ya Kandaga katika kijiji cha Mlela ambapo amewaagiza Shirika la Umeme Tanesco Mkoani Kigoma kufunga mara moja transfoma la Umeme ndani ya siku Tano ili kuwezesha mtambo WA maji kuanza kufanya kazi.
Sambamba na hilo amefanya Mkutano Wa hadhara na wananchi wa Kata ya Nguluka huku akiwataka wananchi hao kujitokeza Kwa wingi tarehe 28 Agosti,2022 kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.
Ameyasema hayo Leo tarehe 06 Agosti,2022 Wilayani uvinza Mkoani Kigoma.