CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


Nukuu Nne Muhimu Za Dkt. Bashiru Ally Katika Uzinduzi Wa Kitabu Cha 'The Game Changer' Chuo Kikuu Dodoma.

alternative

1. "Viongozi bora wana Mapinduzi na wana Mageuzi, huzaliwa lakini pia huundwa  (Good leaders are born and made) kwa hiyo Rais Magufuli ni binadamu kazaliwa, na kiini cha uongozi wake bora ni wazazi wake, walezi na jamii yake."

2. "Rais Magufuli ni tunda la uundwaji wa viongozi bora katika Taifa letu, hivyo kazi za taasisi za elimu, familia, vyama vya siasa, taasisi za dini, na vikundi mbalimbali katika jamii, vina jukumu la kuunda viongozi baada ya kuzaliwa."

3. "Rais Magufuli ninavyomjua katika muda niliofanya naye kazi kama msaidizi wake, sio mtu anayependa sifa, tusije chukulia uzinduzi wa kitabu hiki kama vile tunampamba kumuongezea umaarufu, lakini ana haki ya kusifiwa kwa kazi nzuri aliyoifanya."

4. "Kama viongozi huundwa baada ya kuzaliwa, bila shaka mchango wa CCM katika kumuunda Rais Magufuli kuwa kiongozi bora ni mkubwa na mimi najisikia fahari kuwa na kiongozi hodari anayetokana na CCM, na kazi ya CCM sio kubweteka ni kutafuta namna ya kuendelea kuunda viongozi bora hata baada ya Dkt John Pombe Magufuli."

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50