CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameongoza sherehe za kutimiza miaka 58 ya Mapinduzi ...

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameongoza sherehe za kutimiza miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 12. 1964, zilizofanyika katika uwanja wa Aman Jijini Zanzibar.

Katika sherehe hizo viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali walihudhuria akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa, Marais na viongozi wengine Wastaafu wa Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa Mikoa mitano ya Zanzibar.

Mara baada ya kuwasili uwanjani, Rais Dk. Mwinyi alipokea salamu ya Rais na Mizinga 21 ilipigwa.

Kamanda wa Gwaride alimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kukagua Gwaride.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alipokea Maandamano ya Wananchi na baada ya hapo Gwaride lilipita mbele ya Rais Dk. Mwinyi kwa mwendo wa pole na haraka na kutoa heshima na baadae kupita mbele na kutoa heshima.

Sambamba na hayo, burudani za ngoma za utamaduni kutoka Zanzibar na Tanzania Bara zilitumbuiza.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla alitumia fursa hiyo kutoa neno la shukurani na kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi zake za uongozi sanjari na kuipongeza hotuba aliyoitoa Rais Dk. Mwinyi hapo jana usiku ambayo ni dira katika maendeleo ya Zanzibar.

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50