CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


CHATANDA NA ZAINAB SHOMARI WAMUOMBEA KURA BAHATI NDINGO KUWA MBUNGE WA JIMBO LA MBARALI

alternative

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda *akiambatana na *Makamu Mwenyekiti Zainab Shomari wamemuombea kura Mgombea wa CCM Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bahati Ndingo katika Mkutano wa Hadhara Kata ya Ubaruku.

Akizungumza leo katika Mkutano wa Hadhara ,Mwenyekiti Chatanda amewaomba Wananchi wa Kata ya Ubaruku na wanambarali kwa ujumla kumpigia kura nyingi na zakishindo kwa Mgombea wa CCM ambaye atahakikisha analeta Maendeleo makubwa zaidi ndani ya Jimbo hilo .

" Mimi pamoja na wenzangu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT tumekaa siku sita katika Wilaya hii ya Mbarali tumeonana na wakina mama na wananchi kwa ujumla wa Wilaya ya Mbarali tumeona Jinsi wananchi wa Mbarali wanavyokipenda chama chao hivyo hatuna wasiwasi na wanambarali katika kuichagua chama Cha Mapinduzi ".

alternative alternative alternative

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50