MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM JIMBO LA BUKOMBE MKOA WA GEITA
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo ambae pia ni Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM Jimbo la Bukombe Mkoa wa Geita amepokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020 -2025 Jimbo la Bukombe.
Aidha Ndg. Chongolo ameweka jiwe la Msingi na Uzinduzi wa Jengo la Ukumbi wa CCM wilaya pamoja na Nyumba ya kulala wageni katika eneo la CCM wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Bukombe Ndg Dotto Mashaka Biteko Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini amewaondoa mashaka wanachama wa CCM na kuwasihi waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi, ambapo jimbo la Bukombe lipo salama na maendeleo yaliopo bukombe yanaletwa na wanabukombe wenyewe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo ameambatana na katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni na Mlezi wa Mkoa wa Geita Ndg. Issa Haji Ussi Gavu ambapo ametambulishwa Rasmi leo katika wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita na Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM Jimbo la Bukombe.