CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara katika Jimbo la Kikwajuni, wilaya ya Mjini na Mkoa wa Mjini, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kukagua uhai wa Chama .....

alternative

Kikwajuni,Zanzibar.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara katika Jimbo la Kikwajuni, wilaya ya Mjini na Mkoa wa Mjini, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo.

Katika ziara hiyo, Shaka alitembelea maeneo mbalimbali ikiwamo kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii.

Miongoni mwa maeneo aliyoyatembelea ni pamoja na Kituo cha Afya Raha Leo, ambapo alipata maelezo juu ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali kuboresha huduma kituoni hapo ikiwamo ukarabati na ufungaji wa vifaa vya kisasa. 

Katika mradi huo Shaka alisema CCM inaelekeza kibali cha kituo cha afya Raha Leo kuomba eneo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ghorofa ili waweze kupanua huduma kutokana na ongezeko kubwa la wananchi wanaohudumiwa kituoni hapo kiharakishwe kupatikana ili upanuzi huo ufanyike kwa manufaa ya wananchi.

Pia, alitembelea mradi wa kitega uchumi cha Maskani ya Kisonge ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na wazee kuhusiana na mambo mbalimbali ya kuimarisha uhai wa Chama na mwenendo mzuri wa serikali mbili zinazoongozwa na CCM.

Mbali na hayo, Shaka alikagua tenki la maji katika mradi wa maji Kikwajuni, ambako hata hivyo hakuridhishwa na maelezo ya mradi huo kutokuanza kutoa huduma. Shaka alisema CCM inaelekeza hatua za haraka katika kipindi cha mwezi mmoja zichukuliwe ili mradi huo utoe huduma ya maji safi kama ilivyokusudiwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 ibara ya 186.

Aidha, Shaka alitembelea na kushiriki mkutano wa wanachama kwa Balozi wa Shina Namba 4, Kikwajuni Juu. Akiwa katika shina hili alipokea changamoto ya uhitaji wa mitaji ili wajiajiri hoja ambayo alisema wawakilishi wa wananchi kwa maana ya madiwani, wawakilishi na wabunge pamoja na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali wanalo jukumu la kuwahamasisha wanachama na wananchi kuchangamkia fursa ya uwezeshaji kupitia fedha takribani shilingi bilioni 81 zilizotengwa na Mheshimiwa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kazi hiyo ili waweze kupata mitaji na kufanya shughuli za kuwapatia kipato.

Katika ziara hiyo, Shaka aliambatana na viongozi mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Yusuph Hamad Masauni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Saada Mkuya Salum, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma, wawakilishi, wabunge, madiwani na viongozi mbalimbali wa Chama.

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50