CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


CHONGOLO AWANYOOSHEA KIDOLE WATENDAJI WA SERIKALI,AKEMEA MIGOGORO YA ARDHI.

alternative

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amewataka viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo wanayoyasimamia kiutawala huku akitumia nafasi hiyo lengo la Chama hicho na Serikali kwa ujumla ni kuona changamoto za wananchi zinapatiwa majawabu.

Akizungumza leo na wananchi pamoja na Wana CCM akiwa katika Kata ya Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro Chongolo ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali ambazo zinaendelea kuchukuliwa katika kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi kwenye maeneo husika huku akieleza changamoto kubwa kwenye wilaya ya Mvomero ni migogoro ya ardhi.

“Mimi na wenzangu tumekuja Mvomero kwa ajili ya kuzungumza na wananchi, kusalimiana na kusikiliza changamoto zao.Nimekuja kuhangaika na changamoto za wananchi sio kupiga hadithi, nimepewa changamoto ya migogoro ya ardhi kati ya kijiji na kijiji, Kata na Kata na maeneo ya kiutawala. Changamoto hizi mara nyingi zinasababisha na viongozi ambao wanaongeza maeneo ili kupata kura na baadae anaacha kero kwa wananchi.

“Wakati mwingine inasababishwa na maslahi ya maeneo unaona upande huu wameshamaliza ardhi yao wanataka kukata eneo la wenzao kuhamia kule ili kujinufaisha na mara nyingine ni kwa ajili ya tamaa ya kuuza mashamba, tamaa ya malisho, tamaa ya kulima , na tama zinazoendana na hizo.

Aidha amesema kumekuwepo na utataribu wa kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa ajili ya makazi, kilimo na ugufaji bado kumekuwa kukiibuka changamoto akitolea mfano wakulima wakipewa eneo wanalima hao hao lakini mfugaji akipewa eneo la mifugo anaalika na wenzake baada ya miezi sita anahangaika kutafuta malisho.

Katika Ziara hiyo Katibu mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo ameambatana na Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Ndg. @sophia_mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.

alternative alternative alternative

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50