NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR NDG. MOHAMMED SAID MOHAMMED (DIMWA) AONGOZA MAPOKEZI YA VIONGOZI MBALIMBALI WA VYAMA RAFIKI- ZANZIBAR.
Viongozi mbalimbali wa vyama vilivyokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa kusini mwa Afrika wamewasili Zanzibar na kupokelewa na Viongozi wa CCM wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ndg. Mohammed Said Mohammed (Dimwa) kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kutembelea sehemu za kihistoria ambazo zina mahusiano makubwa na harakati za ukombozi wa ukanda wa kusini mwa afrika.
Ugeni huu umehusisha Viongozi wa Vyama vya Zanu PF (Zimbambwe), SWAPO (Nambia) MPLA ( Angola), na FRELIMO (Mozambique/ Msumbiji) ukiongozwa na Ndg. Anamlingi Macha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.
Viongozi hao wamekagua Kaburi na Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwana Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
Aidha Viongozi hao wamesaini kitabu cha wageni na kuongozwa kukagua Sehemu aliyouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na jengo la Afisi Kuu, ambalo ndilo lilikuwa kituo kikuu cha Mipango ya vyama vya ukombozi wa Afrika.
Vile vile Viongozi wametembelea maeneo mbali mbali ya Kihistoria kama vile kutembelea People’s palace, Ngome Kongwe- Forodhani, Soko la Watumwa - Mkunazini, Jumba la Mawe - Dunga.
Tarehe: 18 Januari, 2023