Chama Cha Mapinduzi

WANACHAMA 200 WA UPINZANI WAOMBA KUJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amesema chama hicho mpaka kufikia jana kilikuwa kimepokea jumla ya wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani 200 wakitaka kujiunga na chama hicho.

Polepole aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za CCM Makao Makuu Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Polepole alisema kwenye kundi hilo la watu mia mbili kuna wabunge kutoka vyama vikubwa vya upinzani, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Viongozi na Maofisa toka Makao Makuu ya vyama vikubwa vya upinzani,madiwani na wanachama wa kawaida.

“Tulikuwa tuwapokee na wabunge na Mameya na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ila kwa sasa tunaweka utaratibu ambapo watapokelewa kwa kishindo mara siku chache zijazo”alisema polepole.

Aidha polepole aliwataka wanachama wapya waliojiunga jana kukijenga chama cha Mapinduzi kwa moyo wote na kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.Fuatilia mtandao wa darmpya.com kwa habari kila zinapotoke

Add comment

Follow us

Don't be shy, get in touch. We love meeting interesting people and making new friends.