Chama Cha Mapinduzi

UN WARIDHISHWA NA UTENDAJI WA SERIKALI YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye pia ni mwakilishi wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez

Umoja wa Mataifa (UN) wafurahia namna Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia suala la Rushwa

Umoja wa Mataifa (UN),umeeleza kuridhishwa na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Rais John Magufuli katika vita dhidi ya rushwa na kupunguza matumizi ya serikali.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye pia ni mwakilishi wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez ametoa taarifa hiyo leo Novemba 7 jijini Arusha.

Amesema rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo katika taifa lolote, kwani rushwa inakosesha huduma bora za afya, rushwa inakwamisha mipango ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwepo elimu na kuleta umasikini.

Hata hivyo, Rodriguez ametaka sekta binafsi kushirikishwa katika mapambano dhidi ya rushwa na kuhakikisha usawa unakuwepo katika jamii, kwa kutolewa ajira zenye viwango pia utunzwaji wa mazingira.

Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na ajira , Anthony Mavunde amesema serikali itaendelea kushirikisha sekta binafsi katika vita dhidi ya rushwa nchini.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na UN na sekta binafsi kuhakikisha inatekeleza malengo 17 endelevu yaliyokubaliwa na Umoja wa Mataifa.

“Tutapiga vita rushwa, tutaendelea kutetea uzawa katika jamii, ajira bora kwa kuhakikisha wafanyakazi wote wanakuwa na mikataba ya ajira lakini pia kutunza nakuhifadhi mazingira ‘’amesema

Awali, Mkurugenzi mtendaji wa sekta binafsi nchini(TPSF), Godfrey Simbeye, amesema sekta binafsi tayari imeanza kushiriki katika vita dhidi ya rushwa na tayari wanachama 60 wamejiunga na mtandao ya kutekeleza malengo endelevu 17 ya umoja wa mataifa.

Hata hivyo, amesema miongoni mwa sababu za rushwa ni urasimu uliopo serikali na kukosekana uwazi katika baadhi ya taasisi.

“Tunajua watoa rushwa wakubwa ni sekta binafsi na wapokeaji ni watendaji waserikali tunaweza kuondoa tatizo hili tukishirikiana pamoja lakini pia tukiondoa vichocheo vya rushwa”amesema

Add comment

Follow us

Don't be shy, get in touch. We love meeting interesting people and making new friends.