Chama Cha Mapinduzi

Rais Kikwete akimtunuku Shahada ya Uzamivu (PhD) Waziri Mwigulu Nchemba

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Shahada ya Uzamivu katika Uchumi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandara.

 

Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Uzamili Katika masuala ya Jiolojia wakifurahia mara baada ya kutunukiwa rasmi shahada hiiyo katika Mahafali ya 47 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia alikuwa amidi wa shughuli za sherehe za chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimkabidhi mrithi wake Profesa Boniventure Rutinwa zana ya kutumikikia nafasi hiyo wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara akitoa neno la shukrani mara baada ya zoezi la kuwatunuku degree zao wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha kufuatia kuhitimu masomo yao kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.

 

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba (kulia) mara baada walipokutana katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Mwigulu Nchemba nimiongoni mwa wahitimu waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Uchumi katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Mlimani City.

 

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamala ya Usimaizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isack. (Picha na MAELEZO)

Add comment

Follow us

Don't be shy, get in touch. We love meeting interesting people and making new friends.